BLANDINA
Stori hii ina muhusu msichana wenye umri ya maika 26 aitwaje Blandina ambaye anazua balaa siku ya maaandalizi ya harusi yake baada ya kukataa kata kata kuvaa shela la harusi..
Binti huyu alisikika akisema : “nataka nivae suruali tena ya kubana ya jeans)”ndugu zake wasijue cha kufanya zaidi ya kulia mpaka wengine wakazimia na kulazwa amana na mihimbili…huku wakihisi mwanao labda atakuwa amelogwa…?
Basi wakaita kundi la wachungaji na mashehe ambao nao maombi yao hayakuzaa matunda,Blandina alishikilia msimamo wake ule ule kuwa katu hato vaa gauni wala sket..anataka suruali…
Je nini kilimfika bint huyu mpaka kuchukia mavazi haya…je ni mapenzi yake au anatatizo fulani ?
Ni siri ndani ya siri ,mikasa ndani ya mikasa..naileta kwenu simulizi hii ya kusisimua upata kuelimika na kuburudika..
Blandina mama…msichana mrembo aliyefanya harusi yake ihairishe mara tatu …kisa tu ni kugoma kuvaa sela..
simulizi inaanza hapa
enjoy..........................
BLANDINA FULL STORY....
Baba lakini ndo nini sasa unafanya…
Wewe tulia usilie mama naweka dawa ya kukufanya kila atakaye kuona avutiwe na wewe pia na uwe na akili darasani sawa mama.
Balndina m zinaniumiza hizo nyembe zako…
Wakati huo wote baba yake balandina alikuwa bize kumuweka mtoto wake dawa maalumu itakayomlinda na kumpa uwezo wa kujulikana kila alipo hivyo.dawa hiyo kwa jina ngwangwa ilikuwa imetoka kigoma na baba yake blandina.walichomwa chale za kutosha wote nyumba zima kuanzia balandina mwenyewe mpaka kaka yake fred,ambaye alikuwa mkubwa kidogo ya blandina na alikuwa form two..
Miaka kadhaa baada baada ya blandina kumaliza form six,alikuwa na hamu kubwa ya kuwa na rafiki wa kiume kwa maana kila waliotongoza walimuacha kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutokewa kubwa ni baba yake blandina kuwatokea usiku na kuwapa maonyo makali kuhusu mwanae.kwa mfano rafiki yake wa kiume samalimfwata na kumwambia
Blandina mama mimi nilikuwa na kupenda sana hata sasa wangu nakupenda ingawa familia yenu ina mambo ya kishirikina mno huwezi amini jama baba yako nimekutana nae mwenge akanisimamisha na kuniambia niachane na wewe ama sivyo atanionyesha na baada ya kusema hivyo akapotea.
Blandina
Baba we koma baba hayupo dar yupo Kenya sasa kajaje mwenge …
Sam
Mama huu ni ukweli kuanzia leo mimi na wewe basi fanya yako nifanye yangu…
Blandina
Ndo milivyo wavulana ukiona umepata wengine basi mapoz mengi sawa..haina shida sam kwa kututukana mimi na familia yangu wachawi….
Sam
Sijawatukana baba yako kanitokea zaid ya mara moja sasa kama sio uchawi ni nini??
Blandina
Hata mimi baba yako alinitokea…m muonee..
Sam
Basi sawa wachawi wameachana…m nimeamua kuokokaaaa
Blandina
Sawa baba kheri….
Sam alikuwa mvulana wa tano kumwambia balandina hivyo katika kipindi cha miaka mine na kitu kilichompa uhakika kuwa baba yake anafanya mambo ya kishirikina ili asiwe na wavulana karibu.ilibidi ampigie simu na kumuuliza na baba yake alikataa katakata kijihusisha na mambo hayo ya kichawi zaid alimsisitiza mwanae asome aachane na hao wavulana hawana cha kumpa.m
Maisha yaliendelea mpaka aakaweza kumaliza shule na kufaulu vyema na kuingia chuo na mwaka wa kwanza alikutana na mvulana ambaye yeye binafsi alirizika naye na kumtaka sana amuoe na kwa kuwa mvulana huyo alikuwa pia anampenda sana blandina alikubali na kuanza utaratibu wakjianda lakini mambo ya ajabu yalianza kumtokea baba yake blandina alianza kumtokea kama kawaida yake na kumpiga biti akae mbali kabisa na mtoto wake..ikabidi siku moja amwambie blandina kuwa kuna mtu huwa anitokea na kuniambia kuwa kama nitajaribu kukuowa tu lazima tutakufa wote..
Blandina kabla hajajibu alianza kulia na kufanya mpenzi wake huyo aliyekuwa anaitwa imam kumuuliza nini mama kuna kitu unakijua sikijui…
Balndina akajibu:hapana baba..
Imam:sasa unalia nini…
Blandina:we niaache kwanza kunakitu nimekumbua mpenzi…
Imam:ok pole dear pole sana..
Immma akaendelea kumbembeleza blandina bila mafanikio kabisa..
Blandina:nakuomba uniache nikapumzike kidogo nyumbani …
Imam:unaenda nyumbani ..vip vipindi vya kesho…
Blandina;nitatafuta mtu anifundishe inabidi niende nyumbani tu…..sijisikii vizuri…
Imam;poa dear ngoja nikusindikize…
Blandina;mmh powa..
Wakiwa njiani hawakuweza kuongea kitu chochote maana blandina alikuwa anauzuni sana na imam alikuwa anamuangalia na anshindwa kuelewa kwa nin taarifa hile imenuuma sana kiasi kile.walipo dika nyumbani kwao mbezi ,imma hakuingia ndani aliishia nje…na kurudi zake chuo..
Nyumbani kwa kina blandina sasa…
Blandina alingia zake ndani na kukutana uso kwa uso na baba yake alikuwa sebuleni anaangalia tv.blandina alipita zake kama hajamuona vile na kuingizake ndani na alipofika chumbani kwake alikusanya kila kilicho chake na kabla hajaondoka gafla aalitoke mama yake na kugonga mlango..
Blandina alifungua mlango na mama yake alishangaa kuona mwanae anapanga nguo bila hata yeye kuwa na taarifa..basi wakaaza zungumza pale
Mama:eeeeh nini wewe tena…..
Blandina:safi shikamooo…
Mama:marahaba sasa unaenda wapi mama
Blandina:naenda kujitegemea..
Mama:eeeh wewe nani kakuambia kuwa unaondoka hapa bila utaratibu…
Blandina:mama mimi ni mtu mzima naweza kuitegema na hakuna anayeweza nizuia..
Mama:oooh washakujaza upepo huko chuo sio mwaka wa kwaza tu unataka kujitengemea…
Blandina:mama nakuomba uniche kwanza …
Mama haya ngoja nikamwambie baba yako maana sasa hii nyumba wakubwa tumekuwa wengi imeshakuwa shida mungu wangu...mama blandina akaelekea sebuleni na wakazungumza kuhusu kuondoka kwa blandina lakini baba yake akamshauri mama yake kuwa bandina anajua anchokitenda sasa muache aende tu sema cha kufanya nenda hapo ndani kachukue milioni 5, umpe ili aweze kupata nyumba zuri ya kukaa..mama blandina akafanya kama alivyoambiwa na baba watoto wake na blandina alizichukua zile pesa na kwenda kupanga vyumba viwili mtaa ya mwenge na huko ndio yalianza mabalaa maana kila alipokuwa nalala alikuwa naota ndoto nyingi za ajabu mara ajikute sebuleni ingawa aalipokuwa analala alila chumbani,blandina alijitahidi sana kwenda kwenye mahubiri na kuombewa na kuanguka mara kadhaa lakini aliporudi tu nyumbani mambo yalikwenda vile vile…
Siku mmoja baba yake alimtokea blandina usiku wa manane na kumuamusha..blandina aliposhituka alipiga kelele baada ya kumuona baba yake inagawa hakuna aliyesikia..
Baba yake akamwambia:mwanangu huwezi kunikimbia hadi kufa kwako wewe ni wangu huwezi kimbia nilishakuwekea kila dawa ya ajabu hata hayo maombezi unayoendaga hayana maana kabisa,maana mimi huwa nawagawia nguvu za miugiza hao watu hawana kitu kabisa kuna mtu mmoja tu hapa Tanzania anweza kukuponya mama,utajiri wangu upo kwako na ukitoa tu huo mfumo na mimi nimekufa na nahakikisha huwezi kuutoa na moja ya njia ya kupunguza nguvu ni zinaa na huwezi kufanya zinaa wanangu mpaka niamue mimi na huwezi kuolewa kabisa mpaka utakapo kufa.akili zako zote nimekupa mimi ndo maana hata usiposoma unafaulu.baada ya kusema hayo baba yake alitoweka zake